Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutumia mfuko uliopo BoT wa trilioni moja kutoa dhamana kwa waagizaji mbolea kwa njia ya hedging/options?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza napenda nianze na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuanza utekelezaji wa kutoa ruzuku kwenye pembejeo za mbolea na zoezi hilo linaenda vizuri sana na wananchi wamepunguziwa mzigo mkubwa kwenye pembejeo za mbolea kupitia hiyo ruzuku pamoja na soko la dunia mbolea kupanda bei kwa kiasi kikubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu; kwa sababu kimuundo Benki Kuu huwa inakopesha mabenki kwa muda mfupi na katika hali hiyo haiwezi kukidhi mahitaji ya mikopo ya kilimo ambayo ni ya muda mrefu. Sasa je, ni kwanini Serikali haioni kuhamisha huo mfuko kutoka Benki Kuu na kwenda Benki ya Maendeleo ya Kilimo, hizo shilingi trilioni moja ziweze kusaidia wakulima? Nashukuru sana. (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Njeza, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Njeza kwa pamoja kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalichukua na kulifanyia tathmini, tukiona kwamba upo ubora wa kufanya hivyo, Serikali itachukua hatua stahiki. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved