Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Lucy Thomas Mayenga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. LUCY T. MAYENGA (K.n.y. MHE. SALOME W. MAKAMBA) aliuliza:- Tatizo la kukatika umeme mara kwa mara katika Jimbo la Kahama Mjini linaathiri sana uzalishaji viwandani hasa ukizingatia Serikali imepiga marufuku kwa baadhi ya viwanda kama vile vya kukoboa mpunga na kusaga mahindi kutofanya kazi usiku:- Je, Serikali ipo tayari kuruhusu viwanda Wilayani Kahama kufanya kazi masaa 24 ili kufidia uzalishaji unaokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokuwa umekatika?
Supplementary Question 1
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Waziri. Kama majibu yalivyo yanadhihirisha kabisa kwamba kuwataka au watu wa Kahama kuendelea na umeme wa jenereta wakati Watanzania wote na yeye mwenyewe anafahamu kwamba Wilaya ya Kahama ni kati ya Wilaya ambazo ni kitovu cha uzalishaji wa chakula especially mchele na kwa jinsi hiyo kuwazuia kwa namna moja au nyingine wasifanye uzalishaji wenye tija. Nimeshukuru amesema kwamba utaratibu umeanza wa kuwapatia umeme wa uhakika. Ningetamani sana kuona kuwa hili linapatiwa ufumbuzi haraka na ningetaka sasa aseme ni lini ambapo umeme huo utapatikana kwa uhakika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, tatizo la kukatika kwa umeme siyo la Kahama peke yake, ni la maeneo mengi sana Tanzania, likiwepo eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ambapo kule mnaamka mnaulizana kwenu upo? Leo umeme upo? Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anaweza kutusaidia kujua kwamba eneo la Kigamboni sasa litaacha kukatiwa umeme kila siku, kila mara especially siku za Jumapili kuanzia lini? Ahsante.
Name
Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Musoma Vijijini
Answer
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwa swali la kwanza la Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, Kahama imeunganishwa kwenye lane ya Shinyanga ambayo msongo wake ni wa KV 33 na sisi tunajua kwamba umeme huo ni mdogo, ulitosha kwa wakati huo lakini siyo kwa sasa. Kwa hiyo kinachofanyika, nadhani hata kabla ya bajeti yangu kwisha, Ijumaa atawaona watu wa TANESCO wako pale, wameondoka leo, wamekubaliana na Mgodi wa Buzwagi, Buzwagi ndiyo iko karibu sana na Kahama. Kwa hiyo, umeme utavutwa kutoka Buzwagi 33 KV kwenda Kahama. Kwa hiyo, huku watakuwa na wa Shinyanga, huku watakuwa na wa Buzwagi, tatizo hilo litakwisha.
Mheshimiwa Spika, mbali ya hilo la umeme kukatika katika, ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote lazima tufanye maamuzi. Tukiwa tunajenga hii miundombinu kuna wakati lazima tuzime umeme. Watu wa upande wa Ziwa Victoria kila Jumapili umeme unakatika, lakini wanatangaziwa kwamba tunajenga miundombinu ya kusafirisha umeme mwingi kutoka Iringa mpaka hapa Dodoma, tunatoka kwenye KV 220 mpaka KV 400. Tunatoka hapa Singida, Shinyanga mpaka Nyakanazi KV 400. Sasa hii tunaizindua Septemba.
Mheshimiwa Spika, sehemu zingine Tanzania nzima, hata ndugu zangu wa Arusha waliokuwa wanasema umeme unakatikakatika, tunajenga kutoka Singida kwenda Arusha KV 400, halafu kutoka Da es Salaam kupitia Tanga kwenda Arusha KV 400. Hiyo ndiyo TANESCO mpya. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved