Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Maulid Saleh Ali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Welezo
Primary Question
MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuzuia Hati za kusafiria kwa Wakandarasi wanaoingia nchini kutekeleza miradi mbalimbali?
Supplementary Question 1
MHE. MAULID SALEH ALI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Kwa kuwa kumekuwa na wakandarasi wengi kutoka nje ambao wanatekeleza miradi yao nchini bila kutekeleza miradi hiyo kwa wakati; je, Serikali haioni haja sasa ya kuweza kudhibiti passport za Wakandarasi hao mpaka watakapomaliza miradi hiyo kwa wakati? (Makofi)
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa maulid Saleh, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tatizo la Wakandarasi kutokutekeleza miradi ni la kimikataba na pia linahusisha mamlaka nje zaidi ya Uhamiaji. Kwa hiyo, hatua za kudhibiti zinaweza kuwa nyingi kulingana na mkataba husika. Hata hivyo, kama nilivyoeleza katika jibu langu katika swali la msingi, kwamba pale ambapo Jeshi la Uhamiaji linahitajika kutumia sheria hii ambayo nimeiorodhesha hapa ambayo inaipa mamlaka kufanya hivyo kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa, kwa misingi ya sheria hii ambayo nimeizungumza, ikihitajika kufanyiwa hivyo; na imeshafanya hivyo mara kadhaa, lakini haiwezi ikatoka ikasema kila mradi ambao haujakamilika, basi twende tukakamate passport bila kufuata utaratibu.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved