Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: - Je, ni lini Ofisi ya TRA itajengwa katika Halmashauri ya Kibondo ili kuzuia biashara holela katika masoko ya ujirani mwema kati ya Tanzania na Burundi?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, halmashauri hii makusanyo yake ya mwaka 2021 ilikuwa bilioni 5.3 kwa mwaka na Jimbo hili la Muhambwe liko mpakani ambapo tuna biashara za ujirani mwema kwenye Masoko ya Mkarazi na Kumshwabure. Je, Serikali haioni ni muda muafaka sasa kujenga TRA ya kudumu lakini pia na kujenda ushuru wa pamoja mpakani ili kudhibiti biashara holela za mpakani? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, wananchi wa Muhambwe wanafuata huduma za leseni Mkoani Kigoma ambapo ni kilomita 240 kutoka Jimbo la Muhambwe. Je, ni lini Serikali itaanzisha huduma za leseni katika Jimbo la Muhambwe ili kuwaondolea adha wananchi hawa wa Muhambwe?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la kwanza, Serikali imelichukua na tutalifanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba ikimpendeza Mheshimiwa Mbunge niambatane naye kwenda kuona hali halisi ya Wilaya ya Kibondo, tuone namna gani tunaweza tukatatua usumbufu huu ambao wanapata wananchi wetu wa Kibondo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved