Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Joseph Kizito Mhagama

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Madaba

Primary Question

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA aliuliza: - Je, ni kwa nini Mfumo wa Stakabadhi Ghalani hautekelezwi kikamilifu kiasi cha kuwawezesha Wakulima kupata fedha wanapohitaji?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninalo swali moja la nyongeza.

Kama Serikali inaamini kuwa Ushirika ndiyo njia bora ya kufikisha huduma za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo, ikiwemo huduma za Stakabadhi za Ghala na pembejeo hasa mbolea. Je, kwa nini Serikali katika msimu huu haikuona haja ya kutumia Vyama vya Ushirika ili kufikisha mbolea za ruzuku kwa wakulima kwa njia ambayo yenye tija zaidi?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mhagama, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza, siyo kwamba tumeviacha vyama vya ushirika, sasa hivi Bodi ya Mazao Mchanganyiko ndiyo inachukuwa mbolea kwa wingi na kukabidhi Vyama vya Ushirika. Sasa hivi tumeanza utaratibu wa kutambua maghala ya Vyama vya Ushirika na Chama cha Ushirika cha Tumbaku cha Mkoa wa Ruvuma kimepewa jukumu la kuanza kupeleka maeneo ambayo sekta binafsi imeshindwa kuyapeleka.

Mheshimiwa Spika, tunaendelea kufanya hivyo, Mkoa wa Rukwa tutashirikiana na Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya wakulima wa mahindi, Kanda ya Ziwa tunashirikiana na Vyama vya Ushirika vya zao la pamba kwa ajili ya kuongeza usambazaji wa mbolea ya ruzuku.