Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwanne Ismail Mchemba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. MARGARET S. SITTA) aliuliza:- Je, ni sababu zipi zinazoifanya Serikali yetu iridhike na utaratibu wenye usumbufu mkubwa unaowataka wakazi wa Tanzania wanaotaka kwenda Uingereza watafute visa kupitia Kenya na Afrika Kusini?

Supplementary Question 1

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa nchi ya Tanzania ilikuwa koloni la Mwingereza na hivyo kuwa na mahusiano mazuri mpaka hivi sasa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuishawishi sasa Serikali ya Uingereza ili waweze kurejesha huduma hiyo hapa nchini?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumweleza Mheshimiwa Mbunge kwamba utaratibu huu mpya wa Serikali ya Uingereza ni wa duniani kote, siyo kwa Tanzania tu. Kwa hiyo, siyo kwamba ni sisi pekee ndio tumebanwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nimweleze tu kwamba kuhamishwa kwa Kituo cha Kuchakata Visa za Uingereza kwenda Pretoria nchini Afrika Kusini hakujaathiri utoaji wa visa. Sana sana kinachotakiwa kwa sasa ni kwamba ujipange mapema, ufanye maombi mapema, lakini kimsingi muda umebaki vilevile, gharama ni zile zile. Kwa hiyo, wao walichofanya ni kupunguza gharama zao za kuchakata visa kwa kuhakikisha kwamba wanaipa Kandarasi Kampuni ya Tele-Performance, badala ya wao wenye kufanya hiyo kazi. Kwa hiyo, namhakikishia tu kwamba hakuna madhara makubwa ambayo yametokea kwa sababu hiyo.