Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL T. AWACK aliuliza: - Je, ni lini itatolewa bei elekezi ya maji katika Karatu ili kuondoa tofauti kati ya KARUWASA wanaouza unit 1 Sh.1,700 na KAVIWASU unit 1 Sh.3,000?

Supplementary Question 1

MHE. DANIEL T. AWACK: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nishukuru Serikali kwa bei elekezi katika eneo la Mji wa Karatu. Pamoja na shukrani hizi nina swali moja la nyongeza. Je, ni lini Serikali itatoa bei elekezi katika maeneo mbalimbali vijijini kutokana na kwamba kwa sasa bei ni tofauti kati ya kijiji na kijiji na hizi bei huwa inaamuliwa na Jumuiya za Maji Vijijini? Je, ni lini Wizara itatoa bei elekezi katika maeneo mbalimbali katika Jimbo la Karatu?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nikushukuru, kubwa ambalo nataka nilieleze Wizara yetu ya Maji eneo la vijijini, tunatoa huduma kupitia Taasisi yetu ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA). Tulifanya tathmini kuona baadhi ya maeneo ya mjini na vijijini unakuta eneo la vijijini walikuwa wakilipa gharama kubwa katika suala zima la ulipaji wa maji. Wizara imeshatoa bei elekezi, ipo miradi ambayo inatumia nishati ya umeme, ipo miradi ambayo inatumia nishati ya jua. Kwa hiyo tumetoa maelekezo kila mradi kutokana na pump zinazotumika imewekwa hela yake rasmi kwa ajili ya kulipa hususan kwa maeneo ya vijijini.