Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sebastian Simon Kapufi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Mjini
Primary Question
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni nini kinakwamisha barabara ya Magamba – Mtapenda – Kasokola hadi Ifukutwa kuhamishiwa TANROADS?
Supplementary Question 1
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana pia nashukuru kwa majibu ya Serikali, ninalo swali moja tu la nyongeza.
Wakati Waziri mwenye dhamana akilisukuma jengo hili, je, Serikali haioni umuhimu wa kuigeuza barabara hii kuwa ya mzunguko au ya pete ili kuepusha Mji wa Mpanda na msongamano wa magari? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba hii barabara ni ya mzunguko kwa maana ya ring road ikiunganisha Halmashauri ya Nsimbo, Mpanda Manispaa pamoja na Halmashauri ya Tanganyika. Kwa hiyo, kwa umuhimu huo tunaitambua na ndiyo maana tunai-push zaidi ili iweze kupandishwa hadhi na iweze kuhudumia watu wote kwa wakati wote. Kwa hiyo, jambo hilo Mheshimiwa Mbunge tumelipokea. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved