Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Vijijini
Primary Question
MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka vifaa kingaradi katika eneo la Mwese lenye milipuko ya radi mara kwa mara?
Supplementary Question 1
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, swali langu la msingi nimeomba kupatiwa vifaa kingaradi kwenye eneo la Mwese.
Je, Serikali ni lini itapeleka hivyo vifaa kwa kuwa, eneo hilo lina radi za mara kwa mara na wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao na mali zao, hasa mifugo?
Mheshimiwa Spika, napenda kupata majibu ya msingi kwa Mheshimiwa Naibu Waziri atueleze vifaa hivyo vitafika lini?
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Selemani Kakoso, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa sababu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 bado unaendelea na sasa tuko katika robo ya pili, namhakikishia Mheshimiwa mbunge kwamba tutahakikisha hii pesa imeenda na kwenye maeneo hayo ya Mwese pia, vifaa hivi vitafika kwa kukamilisha na hiyo miundombinu ya umeme ambayo inahitajika katika maeneo hayo kwa haraka iwezekanavyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved