Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fakharia Shomar Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE.FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Magari yanayobeba abiria nchini yamekuwa yakitozwa faini pindi yanapokamatwa kwa kosa la kujaza abiria zaidi ya uwezo wake badala ya kutakiwa kupunguza abiria waliozidi. (a) Je, Serikali haioni kuwa kutoza faini na kuacha gari liendelee na safari huku likiwa limejaza ni sawa na kuhalalisha kosa? (b) Je, Serikali haioni kuwa ikiwashusha abira waliozidi itakuwa imetoa fundisho na kupunguza ajali kwa abiria ambao hupanda gari huku wakijua limejaa?
Supplementary Question 1
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Ahsante Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri aliyoyatoa, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa ajali zinazotokea huacha athari nyingi mfano vifo, ulemavu, uharibifu wa mali na hata ya mayatima, je, kwa nini Serikali sasa isianzishe Mfuko wa Ajali yaani Accident Fund kwa ajili ya wahanga wanaofikwa na matatizo hayo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili kwa nini wale abiria wanaopanda ndani ya gari ambao umetuambia kwamba mnawashusha na kuwarejeshea fedha zao. Ningeona kwa nini na wao wasingetozwa faini ikawa kama ni sehemu ya wengine kuogopa kupanda magari ambayo watu wamezidi? Wakiona wanatozwa faini najua na wale watakuwa kama kigezo kwamba nikiingia kwenye gari hii na mimi nitatozwa faini wakati gari imejaa? Naomba Mheshimiwa unijibu.
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge ametoa ushauri kwamba tuanzishe mfuko kwa ajili ya wahanga wa ajali hizi lakini pia ametoa ushauri kwamba abiria ambao wamezidi kwenye mabasi nao washitakiwe kwa maana ya kulipishwa faini. Naomba tu nishauri kwamba mapendekezo yake haya mawili niyachukue kwa ajili ya kuyafanyia kazi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved