Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdalla Rashid

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiwani

Primary Question

MHE. RASHID ABDALLA RASHID aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaviwezesha vikundi vya uhifadhi mazingira Vijiji vya Chwaka, Kiwani, Jundamiti, Mwambe, Nanguji na Kendwa?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID ABDALLA RASHID: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali la nyongeza. Ni kweli vikundi vimepatiwa mafunzo haya na vinapatiwa tunzo, lakini ni lini vitapatiwa fedha ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao badala ya kukaa na mafunzo kwa takribani miaka miwili bila kupata fedha? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Abdalla Rashid, Mbunge wa Kiwani, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali tayari imeshafanya mafunzo kwa vikundi hivi vya uhifadhi wa mazingira na tayari tumeshafanya uwezeshaji wa wataalam, hivyo Serikali sasa kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar watafanya uwezeshaji wa vikundi hivi ili viweze kutekeleza miradi hii.