Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZAINAB A. KATIMBA K.n.y. MHE. JULIANA D. MASABURI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapa Vichanja vya kuanikia dagaa Wanawake Wajasiriamali wa Mkoa wa Mara?
Supplementary Question 1
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Kwa kuwa wanawake wa Kigoma wanaojishughulisha na uvuvi wanahitaji kujengewa uwezo katika mnyororo wa thamani na kuongezewa pia mitaji. Je, ni lini Serikali italeta mradi huu ili uweze kuwanufaisha wanawake wa Mkoa wa Kigoma wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi. (Makofi)
Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Answer
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Katimba, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Kigoma, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wa Kigoma na Ukanda wote wa Ziwa Tanganyika, tuna mradi unaoitwa Fish for ACP ambao unajumuisha Ukanda wote wa Ziwa Tanganyika. Lengo la mradi huu ni kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi kwenye Ziwa Tanganyika ikiwemo dagaa, migebuka na mazao mengine ya uvuvi yaliyoko kwenye Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Mradi huu unalenga kuongeza ubora, unalenga kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi unaotokea kwenye mialo na kwenye masoko yalioko kwenye ukanda huo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tayari, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi huu na mwaka huu tutaendelea; na miaka mingine tutaendelea mpaka ukanda uliye...
NAIBU SPIKA: Ahsante kwa majibu mazuri.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved