Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daimu Iddi Mpakate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kupandisha Shule za Sekondari za Mchoteka na Nalasi kuwa za kidato cha tano na kidato cha sita Wilayani Tunduru?
Supplementary Question 1
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Tunduru Kusini lina shule za sekondari kumi, katika hizo zote hamna high school na Shule ya Sekondari Mchoteka ina maabara tatu, ina mabweni mawili na moja linajengwa, ina vyoo 20, kumi na moja vya kike na tisa vya kiume, halafu ina madarasa 16; kati ya hayo manne hayatumiki. Kigezo kilichobaki ni bweni pamoja na jiko.
Kwa nini sasa Serikali kwa kutilia umuhimu wa kutokuwa na high school katika Jimbo langu isitilie mkazo wa kupewa fedha kwa haraka ili Jimbo la Tunduru Kusini lipate high school?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba moja tumepokea ombi lako, kwa sababu kwa kuizingatia hiyo shule itatupunguzia gharama za kwenda kuanzisha high school mpya, kwa hiyo tumelipokea na tutalifanyia kazi ili sasa tulete shule ya Kidato cha Tano na Sita katika Jimbo lako, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved