Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Florent Laurent Kyombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaitengea bajeti barabara inayounganisha Uganda na Tanzania ya Kibaoni - Kakunyu kwenda Bugango mpakani ambayo iko chini ya TARURA wakati taratibu za kupandishwa hadhi zikiendelea ili iweze kupitika wakati wote?
Supplementary Question 1
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba niongezee maswali mawili ya nyongeza: -
Mheshimiwa Spika, barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12 kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri ni ya muhimu sana kwa wananchi wa eneo hilo ikitokea Lubira, Kyabunaga, Bugango mpaka mpakani.
Je, sasa ni lini Serikali itaona umuhimu wa barabara hiyo kwakuwa inakidhi vigezo vyote vya kuhudumia na TANROAD ipandishwe hadhi kwenda kule iwe imepata bajeti ya uhakika?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, barabara ya kutokea Kiwanda cha Kagera Sugar kwenda Kijiji cha Bubali imekuwa ina changamoto kwa muda mrefu na inahitaji matengenezo makubwa.
Je, ni lini barabra hiyo itatengewa bajeti ili iweze kutengenezwa na wananchi waweze kutumia barabara hii? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mbunge ameomba barabara hiyo kupandishwa hadhi na jukumu hilo kubwa linafanywa na wenzetu wa TANROADS, kwa kuwa Serikali ni moja basi sisi tutalipokea hilo ombi ka niaba ya TANROADS na watakwenda kulifanyia kazi kwa kufuata zile taratibu ambazo zinatakiwa.
Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Kagera Sugar kwenda Bubali ambapo ameainisha hapo ni lini itapangiwa fedha, mimi nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba nitawaagiza Maneja wa TARURA wa Wilaya na Mkoa wa Kagera waende wakafanye tathmini ili sisi tutafute fedha kwa ajili ya barabara hiyo. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved