Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Asia Abdulkarim Halamga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE ASIA A. HALAMGA K.n.y. MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: - Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya kusajili na kuboresha miundombinu ya Shule Shikizi zilizojengwa kwa nguvu za Wananchi?
Supplementary Question 1
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali kwa kutenga shilingi 1,140,000,000 kwa ajili ya kujengwa shule 57 katika Jimbo la Kiteto.
Je, Serikali ni lini itaharakisha sasa usajili wa shule hizi ili wananchi waweze kupata huduma kama ambavyo nia ya Mheshimiwa Rais imeweza kulenga kutatua changamoto?
Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kufuatana na Mbunge wa Jimbo la Kiteto ili kwenda kuona hali halisi ya vituo hivi ambavyo vinajengwa kwa sasa?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asia Halamga, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu cha kwanza kabisa niseme kwamba napongeza kazi nzuri anayoifanya, na nimhakikishie tu kwamba Serikali ipo tayari kusajili shule zote ambazo zimekamilika na maeneo yote ambayo yanahitaji. Kwa hiyo, wayafuate tu yale maelekezo ambayo tumeyatoa na sisi tutazisajili.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, niko tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo pamoja na Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kuhakikisha tukajionee hizo kero za wananchi. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved