Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE AIDA J. KHENANI K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isitumie mbao za Mitiki zenye ubora sawa na Mninga/Mkongo kwani tenda za Serikali zinataka Mninga/Mkongo?

Supplementary Question 1

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Sote tunajua kwamba bado kuna changamoto kubwa sana ya madawati hapa nchini na wananchi wamekuwa ni wahifadhi namba moja wa misitu pamoja na miti mingine ambayo inapandwa na Watanzania wenyewe. Serikali ina mpango gani sasa wa kutumia miti mingine ambayo inataka kufanana na mininga ambayo iko maeneo mengi ili kuweza kuondoa changamoto hiyo ya madawati?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kaboyoka, kwa niaba yake ameuliza Mheshimiwa Aida, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza niweze kuifahamisha jamii na Watanzania wote kwamba, Serikali imefanya utafiti wa miti 19 na moja ya utafiti huu ni pamoja na mti wa mtiki. Tunaangalia namna iliyo bora ya kufanya mazungumzo na Wizara ya Fedha kupitia PPRA ili kuwe na mwongozo maalum wa kuhakikisha kwamba miti hii sasa inatumika kwenye furniture. Kwa hiyo nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba changamoto ya madawati ambayo imekuwa ikijitokeza katika jamii inaenda kupungua kwa sababu aina ya miti 19 kama itaenda kutengeneza haya madawati, basi kutakuwa na aina mbalimbali ya miti ambayo ni mizuri na bora na imefanyiwa utafiti na wataalam kutoka Maliasili na Utalii. Ahsante.