Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 1

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza. Bei hii inayosemwa imepanda sasa ilikaa zaidi ya miaka mitano bila kupanda, wakati kwenye Soko la Dunia bei ilikuwa ikipanda ukiacha kile kipindi cha Covid-19: Ni upi mkakati wa Serikali sasa angalau kufanya mapitio kila mwaka ili kuhakikisha kwamba tunawasaidia wakulima wa nchi hii wakiwemo wakulima wa Tarafa ya Bungu kule Korogwe? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Moja ya njia ya kusaidia kupanda kwa bei ya chai ni kuwa na mnada wa kwetu Tanzania. Mheshimiwa Waziri, Serikali ilituahidi tangu mwaka 2019, ukiwa Naibu Waziri, kuanzisha mnada wa chai Tanzania, lakini mpaka leo mnada huo haujaanzishwa: Ni nini kauli ya Serikali juu ya kuanzisha mnada wa chai ndani ya nchi yetu ya Tanzania?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Timotheo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei iliyodumu kwa kipindi cha miaka mitano ni bei ya shilingi 312. Kikao cha wadau kilichofanyika mwanzoni mwa mwaka huu ndicho tulichobadilisha bei na kuipeleka kuwa shilingi 366 kwa maana ya bei ya chini ya chai. Sasa hivi katika baadhi ya maeneo, hasa maeneo ya Nyanda za Juu Kusini wakulima wanauza chai grade one mpaka shilingi 420. Kwa hiyo, mabadiliko ya bei yamefanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu ambalo tunalifanya kwenye eneo la bei, Serikali inapitia mfumo mzima wa uchakataji na importation ya chai kutoka nje ili kuvifanya viwanda vya ndani na kuongeza consumption ya matumizi ya chai ya ndani na kuvipunguzia baadhi ya tozo mbalimbali. Mtaona kwenye bajeti itakapokuja Wizara ya Fedha, mtaona mabadiliko katika eneo hilo ili kuvifanya viwanda vya blending vya ndani viweze kutumia zaidi chai ya ndani na kupunguza importation ya chai kutoka nje na kuvitengenezea soko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mnada. Nataka nilihakikishie Bunge lako, ni kweli, dhamira ya Serikali toka mwaka 2019 ilikuwa ni kuanzisha mnada, lakini nilihakikishie Bunge lako kwa uwezo wa Mungu, mwaka huu mnada utaanza. Tumeshakamilisha masulala ya miundombinu, tumeshakamilisha eneo la maabara, tumeshakamilisha mwongozo, na sasa hivi tuko hatua za mwisho kwa ajili ya kusajili ma-broker wa Kimataifa ambao watashiriki kwenye trading kwa sababu, uuzaji wa chai una utaratibu wake.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza: -

Je, Serikali inawasaidiaje kwa dharura wananchi wa Kata ya Ruaha Mbuyuni, Wilaya ya Kilolo kwa kuwa wameingia taharuki kubwa sana; mfereji umeacha njia, umehama, intake imeachwa peke yake, maji hayapo kabisa: Wananchi hawali, hawalali, maji hayapo kabisa na mashamba yamekauka?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli eneo la Ruaha Mbuyuni mfereji umehama na mto umehama. Kwa hiyo, hatua ambayo Serikali inachukuwa sasa hivi, timu ya Wataalam wa Wizara ya Kilimo tayari iko Mkoani Iringa kwa ajili ya kuliangalia hilo eneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la msingi ambalo nilitaka nilitaarifu Bunge lako na wakulima wa eneo la Ruaha Mbuyuni, tatizo la Ruaha Mbuyuni halitofautiani na tatizo lililokuwepo kwenye maeneo ya Mlenge na Mkombozi. Kila mwaka mvua zikiwa nyingi mto huacha njia. Kwa hiyo, hatua tuliyoamua kama Wizara, tunaenda kulifanyia detailed design na kutangaza baadaye kwa mwaka ujao wa fedha ili ijengwe comprehensive scheme katika lile eneo na tuondokane na hili tatizo la kila mwaka kwenda kufanya repair katika eneo hilo. (Makofi)

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana; je, Serikali ina mkakati gani wa kuweza kudhibiti bei ya kahawa, maana imekuwa ikipanda na kushuka kila mara? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, na siyo tu bei ya kahawa, ni mazao yote bei inapanda na kushuka. Serikali haiwezi kudhibiti bei, bali Serikali jukumu letu la msingi ni kuongeza tija ili kupunguza gharama za uzalishaji ili wakulima waweze kupata faida baada ya gharama zao kupungua. Kwa hiyo, tunachukua hatua mbalimbali za kupunguza gharama za uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, safari hii wakulima wa kahawa wametumia almost asilimia 7.5 ya mbolea yote ya ruzuku iliyosambazwa. Kwa hiyo, ile itawaongezea tija. Mwelekeo wa Serikali ni kuongeza tija kwa kuwapa miche bora ili kuwapunguzia gharama na kuwaongezea uzalishaji waweze kuwa competitive. Hatua ya pili ambayo tunataka kuweka kwenye zao la kahawa ni uhamasishaji wa matumizi ya kahawa ndani ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nchi, tuna-export kahawa kwa wastani wa dola nne, lakini tuna import made coffee kwa wastani wa dola 20. Kwa hiyo, Serikali sasa tunaanza hatua, mtaona kwenye bajeti ya Wizara ya Kilimo, mfano kwenye maeneo ya Kagera tunaanza uwekezaji kwenye Kiwanda cha TANICA ili tuongeze blending na matumizi ya kahawa iliyokuwa processed ndani na kuongeza unywaji wa kahawa ndani ya nchi na kuwaongezea wakulima soko la uhakika na uhakika wa bei.

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 4

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Hali ya hewa ya Tarime na ardhi vinaruhusu kilimo cha zao la chai. Miaka ya nyuma wananchi walikuwa wakilima chai, lakini waliacha kutokana na kutokuwepo na masoko na bei kuwa chini. Sasa kwa mikakati ambayo Serikali imeainisha hapa, nataka kujua, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba inahamasisha na kufufua zai la chai kwa Wilaya ya Tarime ili kuweza kukuza uchumi wa wana Tarime? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Tarime ilikuwa ni eneo mojawapo la uzalishaji wa chai na wananchi waliacha. Siyo Tarime tu, hata Mkoa wa Kagera na wenyewe ulikuwa ni eneo mojawapo la uzalishaji wa chai, na Serikali ilibinafsisha baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji waliopewa maeneo yale walishindwa kuyaendeleza. Kwa hiyo, kama Serikali sasa hivi, kwa mfano, maeneo ya Kagera tumeanza maongezi na mwekezaji aliyeshindwa ili tuweze ku-take over kile kiwanda kupitia ushirika na Serikali kuweza ku-bail out tuweze kufufua chai eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutafanya tathmini economically, kuangalia kama tuendelee na jitihada tunazozifanya kwenye mazao ya chakula na mazao ya kahawa kwenye eneo la Tarime, ama tulilete zao la chai na litatuathiri namna gani? Kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mbunge tutafanya tathmini and then tutakuwa na majibu ya uhakika. (Makofi)

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 5

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nilitaka kujua ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la korosho linarudi katika bei ya miaka ya nyuma ya shilingi 4,000 na kuondokana na bei ya sasa ya kilo shilingi 1,600? Ahsante.

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, njia pekee ya mazao ya kilimo kuwa na uhakika wa bei nzuri kwa mkulima na kuwa na uhakika wa soko ni njia mbili. Moja, kuongeza tija, kupunguza gharama za uzalishaji.

Pili, ni kuongeza thamani katika mazao kwa maana ya value addition na kuacha kuuza mazao yetu ghafi nje kwa sababu tunauza na ajira zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie watu wa korosho, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, 2025/2026 hatuta-export korosho raw, tutabangua zote ndani ya nchi hii. Kuanzia mwaka ujao wa fedha tutatenga kiasi cha Shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuanza safari ya ubanguaji ndani ya nchi yetu kwa kuwasaidia sekta binafsi ya Kitanzania. (Makofi)

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 6

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Moja kati ya sababu zinazowafanya vijana wa Nyanda za Juu Kusini, hususan Mkoa wa Njombe kutokupenda kulima zao hili la chai ni pamoja na bei ya chini ya zao la chai.

Je, ninyi kama Serikali mmejipanga vipi kuhakikisha kwamba mnawa-motivate vijana waweze kushiriki katika kilimo hiki cha chai ikiwa ni pamoja na kuanzisha program za out growers kwenye mashamba ya chai? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli zao la chai siyo vijana peke yake, baadhi ya maeneo wakulima wameanza kuling’oa. Tunapitia upya mfumo mzima wa chai. Ni sahihi kwamba, wakati bei ya chai inapanda ama pale ambapo tunakuwa tegemezi, mfumo wetu wa masoko kwa wenzetu walioko nje ya nchi, maana yake tunakuwa vulnerable siku zote. Kwa hiyo, kama Serikali kama hatua nilizozisema za mwanzo kuanzisha mnada, kuongeza value addition ndani ya nchi, kupunguza importation ya chai kutoka nje, automatically jambo hili litasaidia wakulima kuwa na uhakika wa soko na bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii ni safari, nawaomba wakulima wa chai nchini, Serikali imeanza kuchukua hizi hatua. Nawaomba wasing’oe chai na wale wote waliouziwa viwanda, hasa nyanda za Kaskazini na baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu, tumewaandikia barua wafufue mashamba na kuviendesha vile viwanda. Kama hawawezi tutafute watu wengine watakaoweza kuwekeza katika maeneo hayo.

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 7

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa uzalishaji wa tumbaku chini ya uongozi wako mzuri katika Wizara hii umeongezeka sana maradufu mwaka huu; na kwa kuwa, sasa hivi ndiyo tunaenda kwenye soko na uzalishaji ni mkubwa: Serikali imejipangaje kuisaidia Bodi ya Tumbaku kupeleka classifiers kwa wakati kufanya kazi hiyo ili soko lisichukue muda mrefu sana, wakulima waweze kuuza kwa wakati na wapate hela yao kwa wakati? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Kawawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali tunatumia mfumo wa crop financing. Bodi ya Tumbaku ilikuwa inategemea kampuni ziwape magari na mafuta ili kwenda kwenye masoko. Tumetengeneza utaratibu ambao kama bodi, itapata kipato kutokana na zao lenyewe bila kumuumiza mkulima, lakini wakati huo huo kama Wizara tumeanza utaratibu sasa hivi wa kuwatafutia magari Bodi ya Tumbaku ili waweze kufanya kazi zao vizuri na kufanya usimamizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie tu wakulima wa tumbaku na kuwaomba kwa kuwa tumeanza minada sasa hivi, na minada hii imekuwa mizuri, tumbaku imefika mpaka Dola tatu safari hii kwenye minada na ushindani umekuwa wa wazi, nawaomba tu wakulima wahakikishe wanasimamia suala la ubora na wasichanganye kwenye mitumba takataka kwa sababu zitaenda kutuangushia zao letu. Mwaka huu tunatarajia tumbaku itafika tani 120,000 kutoka tani 60,000.

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 8

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na kwamba zao la korosho limekuwa likiteremka mwaka hadi mwaka, lakini uzalishaji katika Wilaya ya Nanyumbu umekuwa ukiongezeka sana: Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari sasa kufikiria kujenga kiwanda ndani ya Wilaya ya Nanyumbu ili kuhakikisha kwamba korosho zote za Msumbiji na zile za Wilaya ya Nanyumbu zinabanguliwa pale pale Wilayani?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mhata, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, siwezi kumwahidi Mbunge mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba tutaenda kujenga kiwanda Nanyumbu. Bali, approach ya ubanguaji tunayoendanayo ni private sector driven, na tunaenda kuisaidia sekta binafsi ya kwetu ya Watanzania. Tutaangalia economic reasons za wapi kiwanda kikae. Kama kutakuwa kuna sababu ya kuweka kiwanda Nanyumbu, tutafanya hivyo, wala hatutasita, lakini kwa hatua ya kwanza, Korosho Processing Center tutakayoanza kuijenga, tutaijenga katika Halmashauri ya Nanyamba na Serikali imeshaanza kulipa fidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Mbunge, kama Halmashauri yake inaweza kutenga eneo ambalo tutaanza kuliwekea miundombinu kwa ajili ya baadaye, tuanze huo mchakato sasa hivi, lakini sekta binafsi ndiyo itakayoamua ni wapi inataka kiwanda chake kiwepo, nashukuru. (Makofi)

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kusaidia kuongezeka kwa bei ya zao la chai kwa wakulima nchini?

Supplementary Question 9

MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona. Serikali imekuwa na utaratibu wa kuagiza mafuta ya kula nchini, ambayo yameua kabisa soko la mafuta ya alizeti ambayo Mheshimiwa Waziri pamoja na Wizara walihamasisha sana ulimaji wa alizeti. Sasa ni lini Serikali itaacha utaratibu huu ili kulinda bei ya mafuta na alizeti hapa nchini? Ahsante. (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli msimu huu kidogo bei ya alizeti imeshuka kwa mkulima. Tunafahamu kwamba mkulima akiuza alizeti chini ya shilingi 900 mpaka ikafika shilingi 700, maana yake anapata hasara. Kama Wizara, tunashirikiana na wenzetu wa Wizara ya fedha kupitia upya maamuzi tuliyoyafanya mwaka 2022 ya ku- reduce tax ya import ya refined palm oil mpaka kufika asilimia 25, kuiangalia impact yake na athari yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nataka niliambie Bunge lako tukufu, import substitution strategy tuliyofanya kama Serikali na ninyi Waheshimiwa Wabunge ya kusaidia kuwekeza kwenye alizeti, ukiangalia report ya BoT ya mwezi huu wa Machi iliyotoka, inaonesha kwa kiwango gani hatua tulizochukua zimepunguza importation ya mafuta ya kula kwa wakati huu wa uzalishaji wa mafuta ya alizeti yameongezeka.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, hatutaruhusu zao la alizeti kufa kwa sababu Serikali inachukua hatua mbalimbali na tutapitia changamoto hizi zilizojitokeza kwa mwaka huu wa fedha ili kuweza kumlinda mkulima na kuhakikisha nchi inajitosheleza mafuta.