Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Vincent Paul Mbogo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga malambo ya kunyweshea mifugo katika Kata ya Chala, Kate, Myula na Nkandasi Wilayani Nkasi?
Supplementary Question 1
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Nina swali moja tu la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Jimbo la Nkasi Kusini lina idadi kubwa sana ya mifugo na wananchi wa Kata ya Ntuchi pamoja na Chala wameshaandaa maeneo ya ujenzi wa majosho. Je, ni lini Serikali itakuja kujenga majosho hayo?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, natambua kazi kubwa anayoifanya katika ufuatiliaji wa kuhakikisha maeneo yake yanapata majosho pamoja na malambo. Kwa bahati nzuri tulishakaa ofisini na kukubaliana jambo hili kwamba, katika mwaka wa fedha kwa sababu tunaendelea na mazungumzo na Wizara ya Fedha, fedha itakayotoka tutapeleka katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameainisha, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved