Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza: - Je, lini Serikali itaondoa Kijiji cha Ngaresero kwenye eneo la Pori Tengefu la Pololeti baada ya kujumuishwa kimakosa?
Supplementary Question 1
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri Kijiji hiki cha Ngaresero bado kina changamoto kubwa na ndio msingi wa swali la Mheshimiwa Mbunge wa Ngorongoro. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kuambatana na mimi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro kwenda kujionea hali halisi ya kijiji hiki? Ahsante.
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwashukuru na kuwapongeza Wabunge wa Mkoa wa Arusha hususan katika Jimbo hili la Ngorongoro na Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Zaytun. Kama ambavyo Serikali imeendelea kutatua migogoro mbalimbali, mgogoro huu tutaenda kuushughilikia ili tukae na wananchi, tuweze kufikia muafaka na hatimaye pori hili liweze kufikia hadhi iliyotarajiwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved