Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali kuingiza lugha ya alama kwenye mitaala ya elimu nchini?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru na kuipongeza Serikali kwa hatua hii kubwa na muhimu iliyofikiwa kama ambavyo imeelezwa kwenye jibu la msingi. Kwa sababu haya yalikuwa ni maombi na mapendezo ya muda mrefu na mara kwa mara kupitia Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba niishauri Serikali, mapendekezo yaliyoelezwa kwenye jibu la msingi yaweze kuzingatiwa ili kwa siku za usoni lugha ya alama iweze kuwa lugha ya kufundishia na mawasiliano katika nchi yetu ya Tanzania. Ahsante. (Makofi)

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): Mheshimiwa Spika, ndiyo, ushauri huo Serikali imepokea.