Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Faustine Engelbert Ndugulile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigamboni
Primary Question
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: - Je, Serikali ina utaratibu gani wa kufanya mazoezi ya utayari katika uokozi wa ajali majini katika Kivuko cha Kivukoni – Kigamboni?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu haya ya Serikali. Katika dhana hiyo ya utayari katika masuala ya uokozi, Wilaya ya Kigamboni ina matanki makubwa ya mafuta na hatuna gari ya zimamoto wala Kituo cha Zimamoto.
Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba tunakuwa na Kituo cha Zimamoto na gari la Zimamoto? (Makofi)
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina mpango wa kuendelea kuimarisha Jeshi letu la Zimamoto na Uokoaji kwa kulipatia vifaa na utaalam ili kutekeleza majukumu hayo. Kama mazungumzo yetu na wakopeshaji yataenda vizuri, tunaweza kupata magari zaidi ya 150 kwa ajili ya shughuli za Zimamoto na Uokozi.
Mheshimiwa Spika, katika mazingira ya Kigamboni ambayo Mheshimiwa amefanya marejeo yake na umuhimu wa uwekezaji uliopo pale hasa matenki ya mafuta, kipaumbele kitawekwa kuhakikisha kwamba kunapatikana magari ya kuzima moto na kuimarisha Ofisi ya Zimamoto upande wa Kigamboni ili kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi, nashukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved