Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Primary Question
MHE. PROF. KITILA A. MKUMBO K.n.y. MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inawapa elimu ya utunzaji mazingira wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katika vyanzo na njia za mito ili wafanye kilimo bila kuleta athari za mazingira?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. KITILA. A. MKUMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa jibu hilo kwa umakini huo ambao ameonyesha Mheshimiwa Naibu Waziri kwenye jibu lake.
Je, lini atakuja kwenye Mtaa wa Kibangu Kata ya Makuburi ili kushughulikia changamoto ya uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye Viwanda vya EPZA?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, najibu swali kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, nipo tayari kwenda kuona uharibufu ambao umefanyika huko na badala ya hapo kukaa na wamiliki wa viwanda hao na kuwaeleza namna bora ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa wananchi, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved