Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. AHMED A. SALUM aliuliza: - Je, ni lini ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Kata ya Ishololo wilayani Shinyanga utakamilika?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu ya Serikali. Kwa kuwa mradi huu ulianza 2012 na 2013 mkandarasi akaondoka na gharama yake ni takribani bilioni 1.4 je, Serikali inatoa ahadi gani kwa wakazi wa Ishololo Usule? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa mradi huu ni muhimu sana kwa wananchi wa Ishololo Kata ya Usule je, Waziri uko tayari kutembelea mradi huu ukaone ni jinsi gani wananchi wa Ishololo – Usule wanauhitaji wa mradi huu? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, cha kwanza nimuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, kwamba Waziri yuko tayari kufika katika eneo la Ishololo – Usule ili kujionea hali halisi ya huo Mradi. Commitment ya Serikali ni kama katika jibu la msingi lilivyoandikwa kwamba katika mwaka wa fedha huu unaokuja 2023/2024 tutafanya tathimini na utekelezaji wa huu mradi utaanza 2024/2025.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved