Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX K.n.y. MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: - Je, Mkoa wa Dar es Salaam umefaidika vipi na uzalishaji wa madini ya ujenzi yaliyozalishwa katika Mkoa huo?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, Mheshimiwa Kisangi angependa kufahamu ni kwa kiasi gani wananchi kwenye maeneo tajwa wananufaika na uwepo wa madini haya kwa maana ya CSR?

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Stella Ikupa kwa swali lake zuri, kwa sababu manufaa ya wanaokaa katika maeneo yanayochimbwa madini, yako ya aina mbalimbali. Kwa upande wa Serikali kodi zinazokusanywa kutokana na hiyo mirabaha pamoja na ada za ukaguzi zinaingia kwenye Mfuko Mkuu wa Taifa na kuingia kwenye bajeti ambayo kila mwaka Mama Samia anapitisha na miradi mbalimbali ya maendeleo kama barabara, zahanati na shule zinapata fedha hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwa upande wa wawekezaji wenyewe au wenye leseni huwa wanatoa michango kwenye miradi mbalimbali ya jamii katika maeneo hayo, sambamba na kutoa ajira katika maeneo ya migodi. Hivyo, manufaa yapo mengi katika mtizamo huo. Pia wale wanaojiongeza, wanafanya huduma za kuwahudumia wenye migodi kama akina mamalishe wanavyokwenda kupika pale na kutoa huduma mbalimbali.