Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Asha Abdullah Juma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: - Je, lini Serikali itaweka taa za kuongoza magari Igunga Mjini kwenye makutano ya barabara kuu ya Singida – Mwanza ili kuepusha ajali?
Supplementary Question 1
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itahakikisha alama zote muhimu katika barabara kuu za nchi yetu zinawekwa na zinasomeka vizuri?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara zote zinazojengwa kisheria ni lazima ziwekewe alama zote za barabarani kwa sababu hizo ndizo zinazoongoza watembea kwa miguu, lakini pia wanaotumia magari na vyombo vyote vya moto, na kila tunapojenga barabara hizo kwa kweli huwa tunajitahidi kuweka alama.
Mheshimiwa Spika, changamoto ni kwamba kuna maeneo ambayo tukishaweka hizo alama, na hasa zile za vyuma inatokea baadhi ya wananchi huziharibu, hiyo ndiyo changamoto. Lakini pengine nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi kwamba alama zote za barabarani zina umuhimu sana kwa maisha yetu na wale watumia barabara zetu muda wote.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved