Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Vijiji vyote vya Mkoa wa Songwe vinapatiwa umeme wa REA?

Supplementary Question 1

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kama ilivyo Mkoa wa Songwe pia katika Mkoa wa Mtwara kuna vijiji 102 bado havijapatiwa umeme. Nataka kujua Serikali ni lini itavipatia vijiji hivyo umeme?
Swali la pili, kwa kuwa umesema mnafanya mchakato wa kutambua Kata ambazo zina hadhi ya Miji lakini ni Vijiji. Nataka kujua ni lini mchakato huo utakamilika ili watu wapate huduma kwa sababu hata katika Jimbo la Mtwara Mjini kuna baadhi ya Kata mfano Kata ya Naliendele, Kata ya Jangwani na zingine zinaonekana ziko Mjini lakini maisha ya watu wake ni kama wako vijijini, nakushukuru. (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tunza Malapo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, alivyosema kama ilivyosomwa lakini na Mtwara pia tunao Wakandarasi wawili, wanafanya kazi katika Mkoa wetu wa Mtwara na juzi tulikaa kikao na Waheshimiwa Wabunge wa Mtwara tukajadiliana kwa upana namna ya kumaliza haraka kazi hizo, tunaamini kwa mkakati tuliouweka kabla ya Desemba mwaka huu kazi yetu ya kupeleka umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Mtwara itakuwa imekamilika na hilo tunauhakika nalo na tunawahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwa kutupitishia bajeti juzi tutaendelea kusimamiana na wenzetu ili kazi hii iweze kukamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni lini tutamaliza kazi hii, tunatamani hata tuimalize leo lakini kwa sababu ya kutaka kufanya ushirikishwaji mkubwa na kubaini changamoto za maeneo mbalimbali tunaomba mtuongezee muda kidogo halafu baadae tutakuja kusema ni lini tutamaliza ili tuweze kukamilisha hii kazi kwa Pamoja, tusingependa kuikimbiza harafu ikawa kama ya awali ambayo haikuleta majibu tuliyokuwa tunayatarajia kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge.

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Vijiji vyote vya Mkoa wa Songwe vinapatiwa umeme wa REA?

Supplementary Question 2

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naishukuru Serikali kwa kuwa tayari Mkandarasi wa REA katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu ameshasimika nguzo kwenye vijiji vyote yapata miezi minne. Je, ni lini sasa wananchi wale wa Vijiji vya Mbulu Mjini watapewa umeme kwa kuunganishiwa nyaya na kuunganishiwa umeme kwenye makazi yao?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema miradi yote ya REA three round two itakamilika kufikia Desemba mwaka 2023 lakini kwa nyakati tofauti tofauti vijiji mbalimbali vitaendelea kuwashiwa umeme. Kama alivyosema Mheshimiwa Issaay hayo maeneo ambayo tayari wameshasimika nguzo tunatarajia kwenye mwezi mmoja mpaka miwili tayari kazi itakamilika wakati maeneo mengine tunaendelea kuchimba, kusimika nguzo na kuunganisha umeme, lakini ifikapo Desemba kazi yote itakuwa imekamilika.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Vijiji vyote vya Mkoa wa Songwe vinapatiwa umeme wa REA?

Supplementary Question 3

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Vijiji 33 vya Bunda vilipewa umeme kilomita tatu kwa kila kijiji na sasa Mkandarasi amepeleka kilomita moja kwa kila kijiji. Ni lini kilometa mbili zitaongzwa katika vijiji 33 vya Jimbo la Bunda?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwapongeze Wabunge wa Mkoa wa Mara kwamba katika zile lot ambazo Wakandarasi wao tayari wamekamilisha original scope kwa asilimia 100 na Mkandarasi wa Mkoa wa Mara tayari naye yumo katika orodha ile, kwa hiyo tuendelee kusukuma kwa pamoja ili tuweze kukamilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatarajia mwishoni mwa wiki hii wanzetu wa REA watasaini mikataba na wale ambao wamepata nafasi ya kuongeza hizo kilomita mbili ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa bilioni 351 kwa ajili ya kuongeza kilomita mbili kwa kila Kijiji. Tunatarajia wiki hii zitasainiwa na hivyo mwanzoni mwa mwezi unaokuja kazi za kusimika nguzo na kuvuta waya utaanza katika maeneo hayo ambayo nyongeza ya kilomita mbili inaenda kufanyika.

Name

Juliana Didas Masaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Vijiji vyote vya Mkoa wa Songwe vinapatiwa umeme wa REA?

Supplementary Question 4

MHE. JULIANA D. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Swali langu ni dogo. Je ni lini mradi wa kilomita mbili za nyongeza katika mradi wa REA III round two utaanza kutekelezwa katika Mkoa mzima wa Mara?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwa Mheshimiwa Getere nipende kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Masaburi kwamba tunatarajia Ijumaa ya wiki hii wenzetu wa REA watakaa na wakandarasi. Tayari wameshapewa idhini ya kuendelea na maeneo hayo ya kutekeleza kilomita mbili na wakishasaini mikataba mwishoni mwa wiki hii tunatarajia mwanzoni mwa mwezi unaokuja kazi itaanza na kwa kuwa ni kazi ndogo tunatarajia itakamilika pamoja na kazi kubwa mwezi Desemba mwaka huu kwa sababu ni kupeleka line ndogo za kuwasha umeme katika vijiji vyote ambavyo vilikuwa katika REA III round two kwa maana ya kuongeza kilomita mbili kwa kila kitongoji. Nakushukuru.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Vijiji vyote vya Mkoa wa Songwe vinapatiwa umeme wa REA?

Supplementary Question 5

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Nami naomba niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kijiji cha Majengo, ramani ya umeme imepeleka umeme kwenye kitongoji cha Nshepa badala ya makao makuu ya Kijiji. Je Serikali iko tayari kutoa maelekezo katika vile vitongoji 15, makao makuu ya Kijiji cha Majengo yapelekewe umeme mwaka huu?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakunda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitongoji 15 ambavyo tumepata pesa jumla ya shilingi bilioni 357 kwa ajili ya kuongeza vitongoji 15 kwa kila Jimbo, tulisema juzi katika bajeti na nirudie tena, litakuwa ni chaguo la Mheshimiwa Mbunge mwenyewe kuchagua ni wapi hivyo vitongoji 15 apelekewe. Kwa sababu kama anavosema Mheshimiwa Aweso kwamba anayelala na mgonjwa ndiye anajua mihemo yake, tunaamini Waheshimiwa Wabunge mnatambua zaidi mahitaji yako wapi kutuzidi sisi. Kwa hiyo, tuyashirikishana pamoja na ninyi kujua na kutambua ni maeneo gani ya vitongoji viwe vya kipaumbele wakati tukiwa tunaelekea kupata pesa nyingi ili kumaliza vile vitongoji 36,101 ambavyo bado havijapatiwa umeme. (Makofi)

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Vijiji vyote vya Mkoa wa Songwe vinapatiwa umeme wa REA?

Supplementary Question 6

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi nami kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye miradi mingi ya REA katika baadhi ya vijiji hawa Wakandarasi wamekuwa hawawalipi vibarua na kuna malalamiko mengi. Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha hawa Wakandarasi wanawalipa wale vibarua ambao wanafanya kazi hizo?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mwakasaka, tumekuwa na changamoto hiyo ya Wakandarasi ama kuchelewa sana au kutolipa kabisa malipo ya vibarua wanaofanya nao kazi. Tumelichukulia hatua kwa kuwa tunawasiliana na wale watumishi wa hao Wakandarasi na kuwashauri wanapokuwa wanaingia katika engagement hizi watengeneze vikundi na wawasiliane na Ofisi zetu za Serikali zilizopo kwenye maeneo husika ili changamoto inapotokea tuibaini mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mkoa wa Tabora tumeendelea kushughulikia matatizo hayo nasi ofisini tumeshapata watu mara kadhaa ambao wamekuja na tumewapeleka REA pesa yao imeweza kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawaahidi Waheshimiwa Wabunge kwenye maeneo yetu yote wale wote wanaofanya kazi ujira wao halali utalipwa kwa sababu Serikali inamlipa Mkandarasi na Mkandarasi lazima alipe kwa wale vibarua ambao amefanya nao kazi. (Makofi)