Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, lini wananchi waliopitiwa na ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mto Lumakali Makete watalipwa fidia?
Supplementary Question 1
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Jambo la kwanza kwa niaba ya wananchi wa Makete tuishukuru Serikali kwa mradi huu ambao ni mradi mkubwa ambao tayari dermacation imeshafinyaka na sisi wananchi wa Makete tupo tayari kupokea. Utayari wa Serikali kwamba Mwezi wa saba itaanza kulipa fidia kwa wananchi wetu kwa mwaka huu. Maswali yangu mawili ya nyongeza ni yafuatayo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wanaozunguka eneo hili la bwawa wa Vijiji vya Busokelo, Madihani, Bulongwa, Mwakavuta, Itete pamoja na Ruangwa; vijiji hivi vyote sasa hivi shughuli za kiuchumi zimesimama kwa sababu ya dermacation. Sasa tulikua tunaomba kujua;
Je, mko tayari kuturuhusu wananchi waweze kulima yale mazao ambayo yanaweza kuondoka wa mfupi kwa maana ya mahindi, njegere na shughuli zingine ambazo hazichukui muda mrefu, kwa sababu muda huu shughuli zote zimesimama?
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, bwawa hili linahusisha miradi ya ujenzi wa barabara, kwa maana ya kutoka Makete kuelekea Busokelo kwa Mheshimiwa Mwakibete;
Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuhakikisha miundombinu hii inajengwa kwa sababu huu ni mradi mkubwa ambao utapitisha vifaa vingi; Serikali itajenga barabara hizi lini wakati wa utekelezaji wa mradi huo? (Makofi)
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa niaba ya Serikali na mimi nipokee shukurani na pongezi za Wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa ujumla na Mkoa wa Mbeya ambako bwawa linafika hadi Busokelo. Lakini nimuombe Mheshimiwa Sanga aendelee kuwashawishi wananchi watuvumilie kwa sababu tunatarijia kuanza kulipa fidia mwezi unaokuja au labda mwezi unaofuata baada ya hapo. Katika muda mfupi wananchi watapata kile ambacho wanakistahili ili eneo hili waliweze kuliacha kwa ajili ya sasa Serikali kuwa tayari kufanya shughuli zake ambazo ni za uendelezaji wa mradi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimuahidi Mheshimiwa Sanga kwamba wananchi hawatachukua muda mrefu watakuwa wamepata fidia yao na wanaweza wakaendelea kujiendeleza kwenye maeneo yao na maeneo yao. Lakini pembeni ya hilo tutaendelea kujadiliana na tuzungumze. Tunayo experience mbaya, kwamba tunapotoa nafasi kama hiyo wananchi sasa wanarudi moja kwa moja hata baada ya kulipwa fidia wanataka waendelee kubaki kwenye maeneo yao. Kwa hiyo, tutajadiliana na viongozi wa Serikali wa maeneo husika na wewe Mheshimiwa Mbunge ili tuone namna bora ya kuwahudumia wananchi katika kipindi hiki ambacho ni cha mpito
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye eneo la pili, ni kweli tutagenga miundombinu mbalimbali katika maeneo hayo barabara, madaraja kwa ajili ya kubeba mzigo kuhudumia mradi. Na kwa sababu mradi bado haujaanza, plan yetu ni kuanza kulipa fidia tukamilishe mambo madogo madogo halafu tujenge miundombinu kwa ajili ya kuweze kufikia lile eneo. Kwa hiyo kabla ya mradi kuanza mwaka wa fedha ule mwingine unaokuja barabara na maeneo mengine yanayotakiwa kuwekea miundombinu itawekwa ili ihudumie eneo la mradi lakini pia ihudumie wananchi kwa maendeleo yao ya kila siku.
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, lini wananchi waliopitiwa na ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mto Lumakali Makete watalipwa fidia?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona.
Je, ni lini Wananchi wa Kitongoji cha Cheketu, Kijiji cha Somanga Kusini, Wilayani Kilwa watalipwa fidia ya kupisha ujenzi wa miundombinu ya umeme katika eneo hilo?
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la Mheshimiwa Ndulane linahusiana na ujenzi wa mradi wa kujenga kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi Megawatt 350 pale Somanga Fungu, na tayari tumepata mfadhili, mwenzetu wa JICA, tunaendelea na kukamilisha mazungumzo. Tutakapokuwa tayari kumaliza mazungumzo na kujenga mradi wananchi wa eneo hilo watapewa fidia yao. Tuombe Mheshimiwa Mbunge aendelee kutusaidia eneo hilo liendelee kulindwa ili muda wa kulipa fidia utakapofika basi isiwe ni shida kulipa fidia.
Name
Catherine Valentine Magige
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, lini wananchi waliopitiwa na ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mto Lumakali Makete watalipwa fidia?
Supplementary Question 3
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Katika Mkoa wa Arusha maeneo mengi hususan Wilaya ya Monduli umeme wa REA nguzo zimesimikwa nyanyazimeshawekwa lakini mpaka leo wananchi hawajapata umeme;
Je, ni lini sasa wananchi hawa watapata umeme ili waondokane na adha hii kubwa ya kukosa umeme? (Makofi)
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna maeneo mengi ambapo nguzo zimesimikwa na miradi haijakamilika. Katika maeneo aliyoyataja ya Monduli na maeneo mengine Arusha tunaye mkandarasi anayeitwa ambaye tayari yuko kazini anaendelea na kazi. Nimuahidi Mheshimiwa Mbunge Catherine Magige pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine wote kwamba kabla ya Desemba mwaka huu miradi yote ya REA III Round II itakuwa imekamilika na ndugu zetu wananchi wa Monduli na wengine watapata umeme kwa kadri tulivyokubaliana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved