Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Asha Abdullah Juma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: - Je, Serikali inawasaidiaje Wanafunzi wenye mahitaji maalum katika huduma za vyoo kwenye shule za msingi na sekondari nchini?
Supplementary Question 1
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa baadhi ya watumiaji wenye mahitaji maalum baadhi huwa wanasota kwenda kupata huduma: Je, Serikali inaweza kuhakikisha kwamba vyuo na mashule vilivyojengwa hivi karibuni vimewekewa visaidizi maalum kwa watumiaji hawa kufika vyooni?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Asha Abdullah Juma, almaarufu Bi. Mshua, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika taratibu za Serikali, katika kila Halmashauri wako watu wanaitwa Wakaguzi wa Ubora wa Shule zetu. Maelekezo yetu Serikali ni kwamba wakaguzi wote wa ubora wa shule, wapite katika kila shule iliyopo ndani ya Halmashauri zetu kuhakikisha kama hili hitaji au changamoto iliyoelezwa na Mheshimiwa Bi. Asha (Mshua), inafanyiwa kazi, kuhakikisha kwamba walemavu wote au wenye mahitaji maalum wote mahitaji yao yameangaliwa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved