Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, lini Kituo cha Utalii Kihesa Kilolo chini ya Mradi wa REGROW kitaanza kujengwa?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza naishukuru Serikali kwa hatua tuliyofikia. Pia namshukuru Naibu Waziri kwa juhudi kubwa aliyoifanya mpaka mahali tulipofika. Naamini hatakata tamaa, tumalizie kabisa.
Mheshimiwa Spika, maswali yangu mawili ya nyongeza: La kwanza, kwa kuwa sasa Iringa inakwenda kuwa lango la utalii kusini. Ni namna gani Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba tunaingiza tamaduni, mazingiira ya Iringa, watu wa Iringa, vivutio vya Iringa ili viwe sehemu ya kutoa taarifa au picha halisi kwa watalii watakaokuja kusini?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Mmejipanga vipi kuhakikisha kwamba viongozi wakiwepo Waheshimiwa Madiwani wanapewa semina kuhakikisha kwamba wanaupokea utalii kusini? Ahsante. (Makofi)
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza niwataarifu tu wananchi wa Iringa hususan mikoa yote iliyoko kusini mwa Tanzania, kwamba malengo ya Serikali ni kuhakikisha tunatanua wigo kwa masuala mazima ya utalii. Ujenzi wa kituo hiki unaendana sambamba na kutanua wigo wa masuala mazima ya utalii. Kwa hiyo, tuna Hifadhi ya Ruaha katika maeneo yale ya jirani, lakini tutahakikisha tunaunganisha package zote za masuala ya utalii ikiwemo masuala ya utamaduni, masuala ya kihistoria, tunaunganisha na utalii wa wanyamapori. Haya yote yatakuwa yanaunganishwa kwenye package moja ambayo tutaisaidia sasa sekta hii iweze kukua katika maeneo mazima yaliyoko kusini mwa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, kwenye suala lingine hili la viongozi wa kisiasa hususan Waheshimiwa Madiwani, kwa kuwa tunaanzisha kituo mahususi hiki, lazima tutatoa elimu kwa wananchi na viongozi ili nao watusaidie kutoa promotion katika maeneo hayo na pia waweze kutembelea vivutio hivi, kwa sababu tunaamini kiongozi anapofika katika eneo hilo, tayari anawahabarisha hata wengine ambao hawajawahi kufika katika eneo hilo. (Makofi)
Name
Innocent Edward Kalogeris
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, lini Kituo cha Utalii Kihesa Kilolo chini ya Mradi wa REGROW kitaanza kujengwa?
Supplementary Question 2
MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza utalii ukanda wa kusini, Kata ya Kisaki kuna eneo linaloitwa Kisaki Majimoto ambapo kuna chemchemi inayochemsha maji kiasi hata cha kuweza kulifanya yai likaiva, je, Wizara ina mpango gani wa kutambua eneo hilo na kuliingiza katika kivutio cha utalii?
Name
Mary Francis Masanja
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimtaarifu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mkakati wa Wizara ni kuhakikisha maeneo yote ambayo yana vivutio vya kihistoria ikiwemo Majimoto; tuna maeneo mengi ambayo yana majimoto na eneo ambalo anatoka Mheshimiwa Mbunge, lakini tuna maeneo mengine mengi ambayo yana vivutio ambavyo bado hatujaviibua. Tunataka kila Mkoa, kila wilaya angalau mtalii yoyote anayefika katika eneo hilo, basi aweze kuona kivutio kilichopo katika eneo hilo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba mkakati tulionao ni mkubwa, tunachotafuta sasa hivi ni fedha ya kutosha ili mambo yasonge mbele.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved