Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Leonard Haule

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mikumi

Primary Question

MHE. JOSEPH L. HAULE aliuza:- Wanachi wa Mikumi upande mmoja wamebanwa na Hifadhi na upande wa pili ardhi kubwa wamepewa Wawekezaji ambao hawajafanya uendelezaji wowote katika mashamba ya Kisanga, Masanze, Tindiga na hiyo kupelekea wananchi kukosa ardhi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuirudisha ardhi hii kwa wananchi ili waweze kujiletea maendeleo?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Naomba niongeze maswali mawili ya ziada. Serikali iliagiza Wakurugenzi wa Halmashauri waorodheshe mashamba ambayo yametelekezwa na wameshafanya hivyo. Je, ni lini Serikali itakwenda kutupa majibu ya moja kwa moja?
Swali la pili, kwa kuwa kuna wawekezaji wana mashamba makubwa mfano mashamba ya Miombo Estate, Kilosa Estate, SUMAGRO, Isanga Estate ambao wamebadilisha matumizi na kuvunja sheria na utaratibu, Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kuyarudisha mashamba hayo kwa wananchi wa Jimbo la Mikumi? (Makofi)

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli maelekezo yalikwishatolewa kwa Wakurugenzi wote na hasa kupitia katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa ili kuweza kuainisha migogoro yote iliyopo katika maeneo hayo ili Wizara iweze kuchukua hatua mpaka sasa mashamba ambayo tayari yamekwishaainishwa na kuletwa pale Wizarani ni jumla ya mashamba 75, lakini pia tunavyo viwanja 694. Haya yameainishwa ni katika mashamba yale kuanzia mwaka 2002 mpaka 2015 na utoaji wake sasa tayari uko katika process za kawaida.
Mheshimiwa Spika, vile vile kwa wale ambao wameshindwa kabisa kuendeleza na tayari mapendekezo yameshaanza kushughulikiwa kwa ajili ya kubatilishwa kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 tunatarajia pia kuwa kazi hiyo itafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni, kwa sababu haya yako katika utaratibu na maelekezo yamekwishatolewa.
Waheshimiwa Wabunge, ninachowaomba kwa sababu pia kila Mbunge alipata maelekezo hayo ambayo tunawaomba mfanye kazi hiyo kwa kusaidiana na Halmashauri zenu muweze kuleta na kuainisha migogoro yote na siyo migogoro yote inapaswa kuletwa Wizarani kuna mingine ambayo pia inaweza ikamalizwa na ofisi zetu za Kanda kwa sababu tuna ofisi karibu katika Kanda nane nchi nzima. Kwa hiyo, kuna mengine yanaweza yakatatuliwa katika maeneo hayo ilimradi tu taratibu nilizozitaja katika jibu la msingi basi ziweze kufuatwa na Wizara itakuwa tayari kuyashungulikia.