Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 33 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 287 | 2022-05-30 |
Name
Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba kusini
Primary Question
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano katika Kata za Karambi, Mubunda, Ngenge na Rutoro katika Wilaya ya Muleba?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) K.n.y. WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, mnamo mwezi Disemba, 2021 Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ilifanya tathmini ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu katika Kata za Karambi, Mubunda, Ngenge na Rutoro.
Mheshimiwa Spika, Kufuatia tathmini hiyo, kata tajwa zilibainika kuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na hivyo zimejumuishwa katika zabuni inayotarajiwa kutangazwa kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022 kukamilika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved