Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba kusini
Primary Question
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano katika Kata za Karambi, Mubunda, Ngenge na Rutoro katika Wilaya ya Muleba?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri yenye kutia matumaini kwenye hizi kata ambazo kwa kweli zina changamoto kubwa ya mawasiliano.
Je, niombe kupata commitment ya Serikali ni lini sasa kama zimetiwa kwenye mpango, ujenzi wa minara hii utafanyika kwa ajili ya hizo kata tajwa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) K.n.y. WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi minara hii itaanza kujengwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa tutatangaza kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha huu, kwa hiyo, tunaamini mchakato umeshaanza na mara mzabuni atakapoanza basi minara hii itaanza kujengwa kufuata na taratibu za manunuzi ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved