Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 295 2022-05-31

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa barabara ya kilometa tatu kwa kuanzia katika Halmashauri ya Geita?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKAO NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Musukuma Joseph Kasheku, Mbunge wa Jimbo la Geita, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami nyepesi kilomita moja katika eneo la Nzera.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango uliopo ni kuendelea kuweka kwenye mipango na bajeti ya kila mwaka ili kuweza kukamilisha ujenzi wa kilometa tatu ifikapo mwaka 2025.