Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 296 2022-05-31

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuajiri watumishi wa kutosha katika kada za afya na elimu nchini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKAO NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. NDUGAGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka mkakati wa kuendelea kuajiri watumishi wa kada za afya na elimu kwa awamu kwa kutenga vibali vya ajira katika bajeti.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada ya afya na elimu kwa awamu na katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imepanga kuajiri watumishi 7,612 wa kada ya afya na watumishi 9,800 wa kada ya ualimu katika halmashauri zote nchini. Ahsante.