Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 34 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 304 2022-05-31

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: -

Je, Serikali inawasaidiaje wakulima wa parachichi Iringa ili waweze kulima kilimo chenye tija?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwawezesha wakulima wa parachichi Mkoani Iringa na kwa nchi nzima, Serikali inachukua hatua zifuatazo: -

(i) Kuzalisha miche milioni 20 kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuziuza kwa njia ya ruzuku;

(ii) Kufanya utaratibu wa usajili wa wazalishaji wa miche;

(iii) Kuandaa mwongozo wa kusimamia soko la parachichi na kuandaa mfumo wa madaraja;

(iv) Serikali kujenga vituo vya kuhifadhia parachichi la kuchakata na kuhifadhi (common use facility) katika mikoa mitatu kwa maana ya Dar es Salaam, Kilimanjaro - Wilaya ya Hai na Iringa - Wilaya ya Mufindi, Kijiji cha Nyororo).