Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 369 2022-06-10

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza: -

Je, ni lini Kituo cha Afya Makambako kitapata mashine ya X-ray na Ultra Sound?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makambako, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekwishapeleka mashine ya X-ray kwenye Kituo cha Afya Makambako ambayo ilisimikwa kituoni hapo mwezi Machi, 2021 na inatumika.

Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2021 Serikali ilipeleka mashine ya Ultrasound katika Kituo cha Afya cha Makambako na inatumika, ahsante.