Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 43 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 379 2022-06-13

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUDITH S. KAPINGA aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kuchapisha sheria za Tanzania katika nakala ngumu na nakala laini ili kurahisisha upatikanaji wa sheria hizo?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Judith Salvio Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mara tu baada ya Miswada ya Sheria inaposainiwa na Mheshimiwa Rais kuwa Sheria, Serikali imekuwa ikihakikisha nakala laini zinapatikana kwenye tovuti za Wizara na taasisi zake. Vilevile Bunge na Mahakama wamekuwa wakiweka sheria zote ambazo zimetungwa kwenye tovuti zake ili kurahisisha upatikanaji wake. Aidha, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali amepewa jukumu la kuchapisha na kuuza nakala ngumu za sheria ili wananchi waweze kupata nakala sahihi na kwa urahisi.