Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 43 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 381 2022-06-13

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA katika Makao Makuu ya Mkoa wa Songwe?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge Vwawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo mbioni kuanza utekelezaji wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Songwe ambapo tayari eneo lenye ukubwa wa ekari 50 limetengwa. Chuo hicho kinatarajiwa kujengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.99 kupitia mapato ya ndani ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Ujenzi huo unatarajiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/2023. Nakushukuru sana.