Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 43 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 383 2022-06-13

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati kwenye skimu ya kilimo cha mpunga iliyopo Kata ya Bahi, Wilayani Bahi kwani miundombinu yake imechakaa sana na kupelekea upotevu wa maji?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kenneth Ernest Nollo, Mbunge wa Bahi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu katika skimu ya kilimo cha mpunga iliyopo Kata ya Bahi, Wilayani Bahi ili kujua gharama halisi ya ukarabati. Aidha, fedha kwa ajili ya ukarabati huo zitatengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.