Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 43 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 384 2022-06-13

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Bwawa la Umwagiliaji Bonde la Endayaya Tlawi ambapo usanifu wake ulifanyika mwaka 2007?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina wa bwawa la kuvunia maji la Tlawi litakalotumika katika kilimo cha umwagiliaji na Skimu ya Tlawi yenye ukubwa wa hekta 650 zilizopo katika wilaya ya Mbulu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Tlawi na skimu ambapo taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo zinaendelea.