Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Bwawa la Umwagiliaji Bonde la Endayaya Tlawi ambapo usanifu wake ulifanyika mwaka 2007?

Supplementary Question 1

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali, Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Naibu wake pamoja na watendaji wa Wizara ya Umwagiliaji. Kwanza nichukue nafasi hii pia kumwomba Mheshimiwa Waziri je, ni lini atafanya ziara katika eneo hilo la skimu ya umwagiliaji?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Paul Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru kwa shukrani na pongezi. Nimuahidi tu baada ya Bunge la Bajeti tutakwenda pamoja kuangalia mradi huo.