Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 44 Industries and Trade Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara 393 2022-06-14

Name

Amour Khamis Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbe

Primary Question

MHE. KHAMIS MBAROUK AMOUR aliuliza: -

Je, Serikali ina mikakati gani ya kuwasaidia wamachinga ili waondokane na umachinga na kuongeza mapato ya nchi?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khamis Mbarouk Amour, Mbunge wa Tumbe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, wamachinga ni fursa sahihi ya kujenga uchumi, Serikali itaendelea kusaidia wajasiriamali kifedha na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara, miundombinu na kurasimisha wajasiriamali ikiwemo wamachinga. Nakushukuru.