Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 3 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 38 2023-11-02

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la Kahawa ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya kukuza soko la Kahawa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Jimbo la Mlalo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Tasnia ya Kahawa inatekeleza mkakati wa miaka mitano wa Maendeleo ya Tasnia ya Kahawa (2021 - 2025). Moja ya malengo ya mkakati huo ni kuongeza thamani ya kahawa kutoka 7% za sasa mpaka 15% ya kahawa yote inayozalishwa nchini.

Mheshimiwa Spika, katika kupunguza utegemezi wa soko la nje, Serikali imeweka mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya kahawa kwa ngazi ya tatu na ngazi ya nne (tertiary processing).

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Bodi ya Kahawa kwa kushirikiana na Sekta Binafsi iliweka lengo la kuzalisha miche bora ya kahawa milioni 20. Hadi kufikia Juni, 2023 miche 17,866,980 ya kahawa sawa na 89% ya lengo ilizalishwa. Miche hiyo imeanza kusambazwa kwa ajili ya wakulima katika maeneo yanayopata mvua za vuli.