Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 46 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 409 2022-06-17

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafanya marekebisho ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2020 ambazo zinalalamikiwa na wadau wa Sekta ya Uvuvi?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, inaendelea kufanya marekebisho ya Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2020 ili kuboresha shughuli za uvuvi nchini na biashara ya mazao ya uvuvi ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia maoni ya wadau wa sekta ya uvuvi na maoni yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kwenye Vikao kati ya Wizara na Kamati hiyo vilivyofanyika tarehe 30 Machi, 2020 na tarehe 25 Agosti, 2021. Aidha, Marekebisho ya Kanuni husika yanatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2022.