Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 46 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 410 2022-06-17

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya Uvinza?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nashon William Bidyanguze, Mbunge wa Kigoma Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Uvinza ni moja ya miradi ya Mahakama inayotekelezwa katika kipingi mwaka wa fedha 2021/2022 kupitia programu ya maboresho ya Mahakama. Mkandarasi wa ujenzi wa Mahakama hii amepatikana ambaye ni Lucas Construction na kukabidhiwa eneo la ujenzi mwezi Oktoba, 2021. Kazi za ujenzi zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Julai, 2022.