Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 50 2023-11-03

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Kihungu, Mbinga?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Kilimo naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na usanifu na ujenzi wa skimu mbalimbali nchini kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwemo skimu za Sanga Lugalagala, Sanga Mabuni, Mkungwe na Kimbande zilizopo Wilaya ya Mbinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na utambuzi wa maeneo mengine yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya kufanyiwa usanifu na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Kati ya maeneo yatakayofikiwa na wataalamu ni pamoja na Kata ya Kihungu iliyopo Wilaya ya Mbinga.