Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 4 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 57 2023-11-03

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:-

Je, kwa nini ukumbi wa VETA Nyasa haujawekwa vipooza joto?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Stella Martin Manyanya, Mbunge wa Nyasa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshafanya makadirio ya gharama za kufunga vipooza joto katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Nyasa ambapo katika Mwaka huu wa Fedha 2023/2024, Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 20 kwa majengo yote. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 7.5 zimetengwa kwa ajili ya kuwezesha kununua vifaa vitakavyofungwa katika ukumbi huo ili kuondoa changamoto ya joto kali, nakushukuru.