Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 4 Community Development, Gender and Children Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 60 2023-11-03

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha wazee zaidi ya miaka 60 wanaostahili kupata huduma za afya bila malipo wanapata huduma hizo?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge Newala Vijijini, kuhusu za afya bila malipo kwa wazee wa miaka 60 na kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi cha Julai, 2022 mpaka Juni, 2023, jumla ya watu milioni 2.2 wakiwemo wanaume milioni 1.3 na wanawake 735,169 wametambuliwa kuwa ni wazee wa miaka 60 na kuendelea katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara. Kati ya hao, Wazee 585,672 sawa na asilimia 27.65 walithibitishwa kutokuwa na uwezo wa kugharamia huduma za matibabu hivyo Serikali imewapatiwa vitambulisho vya bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kufanya utambuzi wa Wazee wasio na uwezo katika Halmashauri zote nchini ili kuhakikisha wanapata huduma za matibabu zilizolipiwa gharama na Serikali.