Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 4 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 63 2023-11-03

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati Mahakama ya Wilaya ya Urambo?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jacqueline Kainja Andrea, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Tanzania inaendelea kutekeleza mpango wa kuboresha majengo katika ngazi mbalimbali kwa kujenga majengo mapya na kukarabati baadhi ya majengo ya zamani. Aidha, katika mpango huu, jengo la Mahakama ya Wilaya ya Urambo limepangwa kufanyiwa ukarabati mkubwa mwaka wa fedha 2024/2025. Ahsante.