Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 10 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 136 2023-11-10

Name

Michael Mwita Kembaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga kwa mawe Korongo la Starehe ambalo linahatarisha maisha ya wananchi wa Kata ya Nyamisangara, Tarime?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael Mwita Kembaki, Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali itatenga shillingi millioni 280 kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi wa Korongo la Starehe lililopo Mji wa Tarime.